EPL: Sita viwanjani leo EPL: Nimekusogezea uchambuzi wa Huddersfield v Chelsea

LIGI Kuu ya England msimu wa 2018/19 inatarajia kuendelea tena leo kwa mechi sita kupigwa kwenye viwanja tofauti ambapo mchezo mmoja kati ya hiyo utapigwa kwenye uwanja wa John Smith kwa wenyeji Huddersfield kuwakaribisha Chelsea.

The Terriers inaweza kuwatumia Ramadan Sobhi na Adama Diakhaby kwa mara ya kwanza huku ikitarajia kufanya maamuzi ama kumchezesha au la mchezaji aliyesajiliwa kwa mkopo Isaac Mbenza, lakini haitomtumia Erik Durm.

Mchezaji mpya wa Chelsea Jorginho, ambaye amemfuata meneja mpya wa klabu hiyo Maurizio Sarri kutoka Napoli huenda akcheza kwa mara ya kwanza kwenye Premier League.

Goalkeeper Kepa Arrizabalaga anaweza kucheza baada ya kusajili2a akitokea Athletic Bilbao siku ya mwisho wa usajili.

Kiungo Mateo Kovacic pia anaweza kucheza baada ya kuhamia kwa mkopo akitokea Real Madrid wakati washindi wa Kombe la Dunia N'Golo Kante na Olivier Giroud pamoja na winga wa Ubelgiji Eden Hazard na mlinzi wa England Gary Cahill wakiunganishwa baadavya mazoezi wiki hii.

Mechi nyingine za Premier League leo Jumamosi August 11, 2018 ni Newcastle watakuwa wenyeji wa Tottenham wakati Bournemouth wakiwakaribisha Cardiff City.

Fulham watakuwa nyumbani pia kuwakaribisha Crystal Palace huku Brighton wakiwafuata Watford na Everton watakuwa wageni wa Wolves.

DONDOO ZA MECHI

HUDDERSFIELD VS CHELSEA
Uso-kwa-uso

Ushindi wa karibuni kabisa kuupata Huddersfield kwenye ligi vs Chelsea ulikiwa kwenye Ligi Daraja la Pili uliopigwa Stamford Bridge March 1963. Waliwafunga pia October 1954, wakishinda bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa Leeds Road. Licha ya kufungwa  Chelsea ilimaliza msimu kwa kutwaa taji lao la kwanza la ligi.

Huddersfield Town

Ushindi pekee kwenye mechi 10 za mwisho wa ligi msimu uliopita ulikuwa dhidi ya Watford in April (D4, L5). Katika kipindi hicho walifunga mabao matatu pekee. 

Huddersfield imepoteza mechi 10 za Premier League mwaka 2018, nyingi zaidi ya timu yoyote.

Kwa jumla, the Terriers ilifunga mabao 28 msimu uliopita ikiungana na Swansea City huku ikishindwa kufunga bao kwenye mechi 21 kati ya 38

Vijana wa David Wagner walishinda mechi tatu za mwisho za kujiandaa na msimu mpya wakiwafunga Lyon, Bologna na RB Leipzig wakifunga jumla ya mabao manane. 

Laurent Depoitre aliifungia Huddersfield kwenye michezo yote miwili ya Premier League  dhidi ya Chelsea msimu uliopita.

Chelsea

The Blues ipoteza kwa Burnley kwenye mchezo wao wa kwanza msimu uliopita - ni msimu pekee kupoteza mechi kama hiyo katika misimu  19 iliyopita (W15, D3). 

Chelsea haijapoteza mchezo katika safari zao nane za mwisho za Premier League kutembelea Yorkshire (W6, D2) tangu walipochapwa mabao 2-0 na Leeds mwaka 2002.

Maurizio Sarri alipoteza mechi mbili za ufunguzi wa ligi; akiwa na Empoli mwaka 2014 na Napoli mwaka 2015. 

Alvaro Morata amefunga bao moja kwenye mechi 14 za Premier League tangu Boxing Day. 

Kadi tatu nyekundu kati ya tano zilizotolewa kwenye mechi za ufunguzi wa Premier League wameoneshwa wachezaji wa Chelsea: Thibaut Courtois mwaka 2015, Gary Cahill na Cesc Fabregas mwaka 2017.

Willian amehusika kwenye mabao yote matatu ya Chelsea waliposhinda mabao 3-1 dhidi ya Huddersfield msimu uliopita, akifunga bao moja na kutengeneza mabao mawili.

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "EPL: Sita viwanjani leo EPL: Nimekusogezea uchambuzi wa Huddersfield v Chelsea"

Post a Comment

loading...